Henrikh Mkhitaryan
Willian: Guangzhou Evergrande ya China imeripotiwa kuwa iko tayari kutoa kitita cha £50m kwa ajili ya kumsajili nyota wa Chelsea Mbrazil Willian.Guangzhou inayofundishwa na Luiz Felipe Scolari tayari imeshawanasa nyota wengine wakali kama Paulinho na Jackson Martinez.(Daily Mirror)
Mkhitaryan:Arsenal inafikiria kuimarisha kikosi chake kwa kumsajili kiungo mchezeshaji wa Borussia Dortmund Muarmenia Henrikh Mkhitaryan baada ya nyota huo kuonyesha nia ya kuhamia England.Mkhitaryan,25 ameifungia Dortmund mabao 23 na kupika mengine 22.(Daily Mirror)
Wanyama:Leicester City imeripotiwa kuwa itamsajili kiungo wa Southampton Mkenya Victor Wanyama ikiwa kiungo wake mahiri Mfaransa N’golo Kante atatimka mwishoni mwa msimu.(The Mirror)
Hummels:Borussia Dortmund imethibitisha kuwa mlinzi na nahodha wake Mats Hummels,27 amewasilisha maombi rasmi ya kutaka kuhamia Bayern Munich mwishoni mwa msimu huu.(Bild)
Baston:Tottenham imeonyesha nia ya kutaka kumsajili mshambuliaji wa Atletico Madrid anayecheza kwa mkopo Eibar Borja Baston.Baston,23 ameifungia Eibar jumla ya mabao 18 katika mashindano yote msimu huu.(Daily Mirror)
Moubandje:West Ham United itamsajili mlinzi wa kushoto wa Uswisi Francois Moubandje,25 kama mbadala wa mlinzi wake Aaron Cresswell anayewindwa na Liverpool.(The Express)
Agbonlahor:Mshambuliaji Gabriel Agbonlahor amebwaga manyanga ya kuendelea kuwa nahodha wa Aston Villa na kulimwa faini ya £100,000 .
Mustafi:Mabosi wa Liverpool Jumapili ya wiki hii watasafiri kwenda Hispania kukutana na uongozi wa Valencia kwa ajili ya kufanya mazungumzo ya kutaka kumsajili mlinzi wa kati wa kati wa klabu hiyo ya Hispania Shkodran Mustafi.(Radio Esport)
Aubameyang:Manchester United imeiambia Borussia Dortmund juu ya mpango wake wa kutaka kumsajili mshambuliaji hatari wa klabu hiyo MgabonPierre-Emerick Aubameyang mwenye thamani ya £70m.(Daily Mail)
Origi:Mshambuliaji wa Liverpool Divock Origi atakuwa nje ya dimba kwa kipindi cha wiki tatu akiuguza jeraha la mguu alilolipata wiki iliyopita baada ya kuchezewa rafu mbaya na mlinzi wa Everton Ramiro Funes Mori.(Liverpool Echo)
0 comments:
Post a Comment