728x90 AdSpace

  • Latest News

    Friday, April 22, 2016

    SUPER EAGLES YAPATA KOCHA MPYA

    Abuja,Nigeria.

    Chama cha soka cha Nigeria NFF kimemtangaza Salisu Yusuf kuwa kocha mkuu wa muda wa taifa hilo la Afrika Magharibi akichukua nafasi ya Sunday Oliseh aliyejiuzulu mwezi Februari.

    Salisu Yusuf atakuwa akisaidiwa na Imama Amapakabor,Kennedy Boboye pamoja na Alloy Agu na jukumu lao kubwa litakuwa ni kuiongoza Nigeria kucheza michezo miwili ya kirafiki ya kimataifa dhidi ya Mali na Luxembourg hapo mwezi Mei na Juni.

    Uteuzi huo umefanyika siku ya Alhamis baada ya kamati ya ufundi na maendeleo ya NFF kukutana huko Abuja kujadili mustakabali wa soka la nchi hiyo ambalo limeingia katika mgogoro baada ya serikali kuingilia kati majukumu yake.



    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Post a Comment

    Item Reviewed: SUPER EAGLES YAPATA KOCHA MPYA Rating: 5 Reviewed By: Unknown
    Scroll to Top