Coruna,Hispania.
Baada ya kushindwa kupata ushindi katika michezo mitatu mfululizo ya Ligi ya La Liga hatimaye Barcelona imerejea tena katika makali yake ya kutoa vipigo vizito vizito baada ya Jumatano usiku kuichapa Deportivo La Coruna mabao 8-0 ugenini huko Riazor,La Coruna.
Shujaa wa mchezo wa jana alikuwa na mshambuliaji Mruguayi Luis Suarez aliyefunga mabao manne na kutengeneza mengine matatu.
Mabao mengine ya Barcelona yamefungwa na Lionel Messi, Neymar, Mark Bartra na Ivan Rakitic.
Ushindi huo muhimu umeifanya Barcelona iendelee kubaki kileleni na pointi zake 79.Katika mchezo mwingine Atletico Madrid imeifunga Athletic Bilbao bao 1-0 shukrani kwa bao la dakika ya 38 la mshambuliaji Fernando Torres.Atletico pia imefikisha pointi 79.
0 comments:
Post a Comment