Michy Batshuayi
Batshuayi:Liverpool imepanga kuiongezea makali safu yake ya ushambuliaji kwa kumsajili mshambuliaji wa Marseille Mbelgiji Michy Batshuayi mwenye thamani ya £30m.( Daily Mirror )
Gundogan:Kiungo wa Borussia Dortmund Mjerumani Ilkay Gundogan anakaribia kutua Manchester City kwa ada ya £23 na anatarajiwa kusaini mkataba wa miaka mitano wa kuitumikia miamba hiyo ya Etihad.(The Daily Mail)
Carrick:Michael Carrick ameambiwa hatapewa mkataba mpya na Manchester United mpaka hapo kitendawili cha kocha mpya kitakapokuwa kimeteguliwa. ( The Sun )
Forsberg:Everton ina matumaini ya kuwapiku wapinzani wao wakubwa Liverpool katika mbio za kumsajili winga wa Red Bull Leipzig Emil Forsberg.(Daily Express)
Forster:Chelsea imeripotiwa kuwa itamsajili mlinda mlango wa Southampton Fraser Forster ikiwa mlinda mlango wake namba moja Thibaut Courtois ataamua kujiunga na Real Madrid. (Daily Mail)
Arteta:Kocha wa Tottenham Muargentina Mauricio Pochettino anamtaka nahodha wa Arsenal Muhispania Mikel Arteta kuwa sehemu ya benchi la ufundi la klabu hiyo inayopambana kutwaa ubingwa wa ligi kuu England.( Daily Telegraph )
Abdennour:Chelsea inajiandaa kutuma ofa ya kumsajili mlinzi wa kati wa Aymen Abdennour baada ya mlinzi huyo wa zamani wa Monaco kushindwa kupata nafasi kikosi cha kwanza cha miamba hiyo ya La Liga.(Tuttomercatoweb.com)
Ben Arfa:Paris Saint-Germain imeripotiwa kuanza mikakati ya kumsajili Hatem Ben Arfa baada ya winga huyo wa zamani wa Newcastle United kufanya vizuri akiwa na klabu yake ya sasa ya Nice.(L'Equipe)
0 comments:
Post a Comment