Dar es salaam,Tanzania.
Hatimaye Yanga imerejea kileleni mwa ligi kuu ya Vodacom Tanzania Bara baada ya jioni ya leo kuibuka na ushindi wa bao 1-0 dhidi ya Mtibwa Sugar katika mchezo mkali wa ligi kuu uliopigwa jioni ya leo katika dimba la Uwanja wa Taifa,Dar es salaam.
Bao lililoirejesha Yanga kileleni limefungwa kipindi cha pili na winga Simon Msuva dakika ya 47 kwa mkwaju mkali wa mita 28.4 akiunganisha pasi ya kiungo Haruna Niyonzima.
Kufuatia ushindi huo Yanga imeiengua Simba SC kileleni baada ya kufikisha pointi 59 katika michezo 24.Simba SC iko nafasi ya pili na pointi zake 57.
0 comments:
Post a Comment