728x90 AdSpace

  • Latest News

    Saturday, April 30, 2016

    MACDONALD MARIGA AFUNGIWA MECHI TANO ITALIA KWA KUMJERUHI MWAMUZI.

    Latina,Italia.

    KIUNGO wa kimataifa wa Kenya anayekipiga katika klabu ya Latina ya Italia Macdonald Mariga amefungiwa kutocheza michezo mitano ya ligi ya Seria B kwa kosa la kumjeruhi mkononi mwamuzi baada ya kulimwa kadi nyekundu.

    Mariga,29 alifanya dhambi hiyo siku ya Jumapili katika mchezo ambao klabu yake ya Latina ilichapwa bao 1-0 nyumbani na Virtus Entella.

    ILIVYOKUWA!!

    Dakika ya 96 Mariga alilimwa kadi nyekundu kwa kumchezea rafu mbaya mchezaji mmoja wa Virtus Entella.

    Kabla hajatoka uwanjani, Mariga alimfuata mwamuzi na kumpa mkono kama ishara ya kumwambia asante, ghafla akaukamata mkono wa mwamuzi huyo na kuuminya kwa nguvu kitendo kilichomsababishia maumivu makali mwamuzi huyo hata kupelekea mkono huo kuvilia damu.

    Kama hiyo haitoshi Mariga alimvurumishia mvua ya matusi ya nguoni mwamuzi huyo hali iliyofanya chama cha soka cha Italia kimlime adhabu hiyo kali.

    Kabla ya kutua Latina Mariga aliichezea Inter Milan mwaka 2010 na kuisaidia kutwaa ubingwa wa ligi ya mabingwa Ulaya kabla ya mwaka 2014 kutua Parma.

    Latina iko nafasi ya 17 katika msimamo wa ligi ya Seria B pointi moja juu ya mstari wa kushuka daraja ikiwa imebakiza michezo minne ya kujitetea.


    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Post a Comment

    Item Reviewed: MACDONALD MARIGA AFUNGIWA MECHI TANO ITALIA KWA KUMJERUHI MWAMUZI. Rating: 5 Reviewed By: Unknown
    Scroll to Top