Pemba,Zanzibar
KOCHA mkuu wa Simba SC Mganda Jackson Mayanja amefichua siri ya kukipeleka Zanzibar kikosi chake kabla ya wikendi hii kuvaana na Azam FC katika mchezo wa ligi kuu Tanzania Bara.
Mayanja amesema ameamua kuweka kama visiwani Zanzibar kujiwinda na mchezo dhidi ya Azam FC baada ya viwanja vingi vya kufanyia mazoezi vya Dar es Salaam kujaa maji kutokana na mvua kubwa zinazoendelea kunyesha jijini humo katika kipindi hiki.
"Tumeamua kuja kuweka kambi huku ili kukwepa mvua Dar es salaam.Tumehofia mvua kuharibu programu zetu za mazoezi"
Jumapili jioni Simba SC itashuka katika dimba la uwanja wa taifa jijini Dar es Salaam kuvaana na Azam FC katika mchezo wa ligi kuu unaotarajiwa kuwa wa vuta nikuvute kutokana na timu zote kuwa katika nafasi nzuri ya kutwaa ubingwa.
0 comments:
Post a Comment