London,England.
Arsenal imejiweka katika mazingira mazuri ya kukata tiketi ya kushiriki michuano ya ligi ya mabingwa Ulaya baada ya Alhamis usiku kuchomoza na ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya West Bromwich Albion.
Ikicheza nyumbani katika dimba lake la Emirates lililokuwa na watazamaji wachache,Arsenal ilionekana kuwamudu vyema wapinzani wao West Bromwich Albion na kufanikiwa kupata bao la kuongoza mapema kabisa dakika ya 6 tu ya mchezo baada ya pasi nzuri ya Aaron Ramsey kumkuta Alexis Sanchez aliyemfuka kiufundi mlinda mlango Ben Forster.
Dakika ya 38 Alexis Sanchez aliifungia Arsenal bao la pili kwa mkwaju wa faulo na kuifanya Arsenal ipae mpaka nafasi ya tatu ikiwa na pointi zake 63 na kuiishusha Manchester City mpaka nafasi ya nne na pointi zake 61 katika michezo 34.
Ushindi huo dhidi ya West Bromwich Albion umekuwa ni ushindi wa 500 kwa Arsenal katika michezo ya ligi kuu England huku Alexis Sanchez akifanikiwa kufikisha mabao 16 msimu huu.
0 comments:
Post a Comment