Manchester,England.
Yaya Toure ataikosa nusu fainali ya kwanza ya ligi ya mabingwa wa Ulaya kesho jumanne wakati timu yake ya Manchester City itakapokuwa nyumbani Etihad kupepetana na Real Madrid kutokana na kuwa majeruhi.
Akitanabaisha habari hiyo kocha mkuu wa Manchester City Manuel Pellegrini amesema amelazimika kumuondoka kikosini Toure baada ya kushindwa kupona kwa wakati jeraha la misuli alilolipata Jumamosi katika mchezo wa ligi kuu dhidi ya Stoke City ulioisha kwa Manchester City kushinda kwa mabao 4-0.
Mbali ya Yaya Toure pia Manchester City itamkosa winga wake Mfaransa Samir Nasri kutokana na kutokuwemo katika orodha ya wachezaji waliosajiliwa kwa ajili ya michezo ya ligi ya mabingwa Ulaya.
Wakati huohuo Pellegrini amesema kikosi chake kimepata ahueni baada ya jopo la madaktari kumtangaza mlinzi na nahodha wake Vincent Kompany kuwa yuko fiti kwa asilimia mia moja na atakuwemo katika mchezo huo muhimu hapo kesho.
0 comments:
Post a Comment