Liverpool, England.
SHIRIKISHO la vyama vya soka barani Ulaya UEFA leo limetangaza kumfungia kwa kipindi cha awali cha siku 30 mlinzi wa Liverpool Mfaransa Mamadou Sakho baada ya hivi karibuni kumkuta na hatia ya kutumia madawa yaliyopigwa marufuku michezoni
Hatua hiyo ya UEFA imekuja baada ya jana Jumatano Sakho,25 kutangaza kuwa hatakata rufaa na wala hataomba kufanyiwa vipimo vingine vya afya.
Taarifa zaidi zinasema UEFA itarefusha zaidi adhabu hiyo pindi uchunguzi wa kadhia hiyo utakapokuwa umekamilika.
Mapema wiki iliyopita Liverpool ilitangaza kumfungia Sakho kwa kipindi kisichojulikana kufuatia vipimo vyake vya afya alivyofanyiwa na UEFA Machi 17 mwaka huu katika mchezo wa Europa Ligi dhidi ya Manchester United kuonyesha kuwa nyota huyo alitumia dawa iitwayo Fat baner ambayo ni maalumu kwa ajili ya kuyeyushia mafuta mwilini na kupunguzia uzito.
Tukio kama hili liliwahi pia kumkuta nyota mwingine wa Liverpool Kolo Toure mwaka 2011wakati huo alikuwa akiichezea Manchester City.Toure alifungiwa kwa kipindi cha miezi sita baada ya kukiri kuwa alitumia madawa yaliyopigwa marufuku.
0 comments:
Post a Comment