London,England.
Arsenal imeshindwa kupata ushindi kwa mara ya pili mfululizo katika muendelezo wa michezo ya Ligi Kuu England baada ya jioni ya leo kulazimishwa sare ya bao 1-1 nyumbani Emirates na Crystal Palace.
Arsenal ndiyo ilikuwa ya kwanza kupata bao la kuongoza dakika ya 44 baada ya Alexis Sanchez kufunga kwa kichwa akiunganisha pasi ya kudokoa toka kwa Danny Welbeck.
Mabadiliko yaliyofanywa na kocha wa Crystal Palace Allan Pardew ya kumuingiza Emmanuel Adebayor yalizaa matunda baada ya raia huyo wa Togo kutoa pasi nzuri kwa Yannick Bolasie aliyewasawazishia bao Crystal Palace kwa mkwaju mkali dakika ya 81 na kufanya mchezo kuisha kwa sare ya bao 1-1.
Kwa matokeo hayo Arsenal imeshuka mpaka nafasi ya nne baada ya kufikisha pointi 60 ikizidiwa na Manchester City kwa idadi ya mabao ya kufunga na kufungwa.
0 comments:
Post a Comment