728x90 AdSpace

  • Latest News

    Sunday, April 17, 2016

    LECEISTER CITY YAPUNGUZWA KASI ENGLAND,VARDY ABOA

    Leceister,England.

    Mbio za Leceister City kuelekea kutwaa ubingwa wa kwanza wa Ligi Kuu England leo mchana zimegonga mwamba baada ya kulazimishwa sare ya kufungana mabao 2-2 nyumbani na Westham United.

    Leceister City ndiyo waliokuwa wa kwanza kuliona lango la Westham United baada ya Jamie Vardy kufunga bao dakika ya 18 akimalizia pasi safi ya NG'olo Kante.

    Mpaka mapumziko matokeo yalikuwa 1-1.Kipindi cha pili kilianza kuwa kibaya kwa wenyeji Leceister City baada ya mshambuliaji wake mahiri Jamie Vardy kulimwa kadi nyekundu baada ya kujiangusha katika lango la Westham United akitaka kumhadaa mwamuzi atoe penati.

    Dakika ya 84 Westham ilipata bao la kusawazisha kupitia kwa Andy Carroll aliyefungwa kwa mkwaju wa penati baada ya Wes
    Morgan kumwangusha Winston Reid. Kuingia kwa bao hilo kuliiamsha Westham ambayo ilikuja juu na kuongeza la pili dakika ya 86 kupitia kwa mlinzi Aaron Cresswell.

    Mchezo ukiwa unaelekea kuisha Leceister City ilifanikiwa kupata bao la kusawazisha kwa mkwaju wa penati kupitia kwa Leonardo Ulloa.Mkwaju huo ulipatikana baada ya Jeff Schlupp kuangushwa na Andy Carroll katika eneo la hatari.


    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Post a Comment

    Item Reviewed: LECEISTER CITY YAPUNGUZWA KASI ENGLAND,VARDY ABOA Rating: 5 Reviewed By: Unknown
    Scroll to Top