728x90 AdSpace

  • Latest News

    Monday, April 18, 2016

    ARSENAL YAPIGA STOP MICHUANO YA KOMBE LA EMIRATES CUP


    London,England.

    Arsenal imetangaza kusitisha kwa muda michuano yake ya kombe la Emirates Cup.

    Akitoa taarifa hiyo Mkurugenzi Mtendaji wa klabu hiyo Ivan Gazidis amesema hatua hiyo imefikiwa ili kupisha ratiba ya michuano ya Ulaya (Euro 2016) pamoja na kutoa nafasi kwa uwanja wa Emirates kufanyiwa marekebisho katika sehemu yake ya kuchezea (Pitch).

    Gazidis amewataka radhi mashabiki wa Arsenal walioko England na sehemu nyingine na kusisitiza kuwa michuano hiyo itaendelea tena mwaka 2017.

    Hii ni mara ya pili kwa Arsenal kusitisha michuano hiyo,mara ya kwanza ilikuwa ni mwaka 2012 ambapo ilisitishwa ili kupisha michezo ya Olympiki iliyokuwa ikifanyika nchini England.

    Michuano ya Emirates Cup ilianza kutimua vumbi lake mwaka 2007 na kwa kawaida hushirikisha jumla ya timu nne kutoa mataifa mbalimbali ya Ulaya.


    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Post a Comment

    Item Reviewed: ARSENAL YAPIGA STOP MICHUANO YA KOMBE LA EMIRATES CUP Rating: 5 Reviewed By: Unknown
    Scroll to Top