728x90 AdSpace

  • Latest News

    Saturday, April 30, 2016

    WELBECK AIPELEKA ARSENAL NAFASI YA TATU ENGLAND

    London,England.

    Danny Welbeck ametokea benchi na kuipa Arsenal ushindi wa bao 1-0 dhidi ya Norwich City katika mchezo mkali wa ligi kuu England ulioisha hivi punde katika dimba la Emirates jijini London.

    Arsenal ambayo kabla ya mchezo wa leo ilikuwa imeshindwa kupata ushindi katika michezo miwili iliyopita ya ligi kuu imepata bao hilo la pekee dakika ya 58 ya kipindi cha pili kupitia kwa Danny Welbeck.

    Welbeck alifunga bao hilo kwa shuti la kudundisha baada ya kupokea pasi safi ya kichwa toka kwa Oliver Giroud na kuipeleka Arsenal mpaka nafasi ya tatu baada ya kufikisha pointi 67 baada ya kushuka dimbani mara 36,nafasi ya nne imekaliwa ma Manchester United yenye pointi 64 baada ya kucheza michezo 35.



    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Post a Comment

    Item Reviewed: WELBECK AIPELEKA ARSENAL NAFASI YA TATU ENGLAND Rating: 5 Reviewed By: Unknown
    Scroll to Top