728x90 AdSpace

  • Latest News

    Sunday, May 01, 2016

    BARCELONA YAKARIBIA UBINGWA WA 24 WA LA LIGA, YAICHAPA BETIS 2-0 UGENINI VILLAMARIN


    Betis,Hispania.

    Barcelona imeukaribia ubingwa wake wa 24 wa ligi ya La Liga baada ya usiku wa leo kuichapa Real Betis mabao 2-0 ugenini huko katika dimba la Benito Villamarin.

    Mpaka mapumziko hakuna timu iliyokuwa imefanikiwa kuuona mlango wa mwenzie.

    Kipindi cha pili Real Betis iliyokuwa pungufu baada ya mlinzi wake Heiko Westermann kuonyeshwa kadi ya pili ya njano dakika ya 35 kwa mchezo mbaya ilishindwa kuhimili tambo baada ya Ivan Rakitic kuifungia Barcelona bao la kuongoza dakika ya 50 baada ya kipa wa Betis Antonio Adan kuchanganyana na mlinzi wake German Pezzella.

    Dakika ya 81 Luis Suarez alifunga bao lake la 35 la La Liga baada ya kupokea pasi toka kwa Lionel Messi na kuifungia Barcelona bao la pili na kuifanya ifikishe pointi 85 baada ya kushuka dimbani mara 36.

    Kwa matokeo hayo Barcelona inahitaji kushinda michezo yake miwili iliyobaki dhidi ya Espanyol na Granada ili iweze kutwaa ubingwa wa La Liga kwa mara ya pili mfululizo.

    Katika michezo ya mapema Real Madrid imeichapa Real Sociedad bao 1-0 huko Anoeta kupitia kwa Gareth Bale.Atletico Madrid wameifunga 1-0 Rayo Vallecano kupitia kwa Antoine Griezmann.



    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Post a Comment

    Item Reviewed: BARCELONA YAKARIBIA UBINGWA WA 24 WA LA LIGA, YAICHAPA BETIS 2-0 UGENINI VILLAMARIN Rating: 5 Reviewed By: Unknown
    Scroll to Top