Antalya,Uturuki.
BAO la kichwa la dakika ya 31 la mshambuliaji wa zamani wa Arsenal Lukas Podolski limeipa Galatasaray ubingwa wa pili mfululizo wa kombe la Turkiye Kupasi baada ya kuwachapa wapinzani wao wa jadi wa jijini la Istanbul Fenerbahce katika mchezo wa Fainali uliochezwa Alhamis usiku huko Antayla.
Podolski,30, alifunga bao hilo akiunganisha mpira wa kona uliotoka kwa Emre na kupalazwa na mlinzi Jason Denayer na kuiandikia Galatasaray bao hilo la pekee na la ushindi.
Fenerbahce imeendeleza unyonge kwa vilabu vikubwa na Uturuki kwani haijawahi kushinda mchezo wowote pindi inapokutana na vilabu vya Galatasaray na Besiktas katika michezo ya fainali.
Fenerbahce imefungwa mara 4 na Galatasaray katika fainali huku pia ikifungwa na Besiktas mara 3 katika fainali.
VIKOSI
Fenerbahce (4-2-3-1): Fabiano; Sener,
Kjaer, Ba, Hasan Ali; Topal, Souza; Alper,Nani, Volkan; Van Persie.
Galatasaray (4-2-3-1): Muslera; Semih,
Denayer, Hakan Balta, Carole; Selcuk, Emre;Sinan, Sneijder, Yasin; Podolski.
0 comments:
Post a Comment