728x90 AdSpace

  • Latest News

    Saturday, May 28, 2016

    NYOTA WA ZAMANI WA MAN UNITED KUBURUZWA MAHAKAMANI KWA UCHOCHEZI


    Paris,Ufaransa.

    NYOTA wa zamani wa Manchester United Mfaransa Eric Cantona anatarajiwa kuburuzwa mahakamani muda wowote kuanzia sasa kwa kile kinachodaiwa kuwa ni kutoa kauli ya uchochezi dhidi ya kocha wa timu ya Taifa ya Ufaransa Didier Deschamps.

    Hatua hiyo imefikiwa baada ya mapema siku ya Alhamis Cantona,kuliambia gazeti la The Guardian kuwa Deschamps amechagua kikosi cha timu ya Taifa ya Ufaransa Kibaguzi.

    Cantona amedai Deschamps hakuwajumuisha kikosi kwa makusudi wachezaji Hatem Ben Arfa na Karim Benzema kwasababu wana asili ya Afrika.

    Amesema " 'Benzema ni mchezaji mzuri'', ''Ben Arfa pia ni mchezaji mzuri.Lakini Deschamps,ana jina la
    Kifaransa.

    ''Pengine ni yeye pekee nchini Ufaransa
    ambaye ana jina la Kifaransa.Ben Arfa ndiye mchezaji bora kwasasa Ufaransa,lakini hayumo kikosini.

    Naye Wakili Deschamps,Carlos Brusa wameamua kwenda mahakamani ili kusafisha jina la mteja wake ambalo limechafuliwa kwa tuhuma za ubaguzi.


    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Post a Comment

    Item Reviewed: NYOTA WA ZAMANI WA MAN UNITED KUBURUZWA MAHAKAMANI KWA UCHOCHEZI Rating: 5 Reviewed By: Unknown
    Scroll to Top