728x90 AdSpace

  • Latest News

    Sunday, May 29, 2016

    HIZI HAPA HABARI KUBWA ZA USAJILI TOKA BARANI ULAYA JUMAPILI YA LEO MEI 29,2016

    Pierre Emerik Aubameyang 

    Nainggolan:Kiungo wa AS Roma Mbelgiji Radja Nainggolan,28 amegoma kuhamia Chelsea katika kipindi hiki cha usajili ili kusubiria kuona kama Kocha Manchester United Mreno Jose Mourinho atamhitaji.(La Gazzetta dello Sport)

    Zieler:Mabingwa wa Ligi Kuu England Leicester City wameshinda mbio za kumuwania kipa wa Hanover 96 na mshindi wa kombe la dunia Mjerumani Ron-Robert Zieler.Zieler,27
    atafanyiwa vipimo vya afya kesho Jumatatu kabla ya kumwaga wino kwa ada ya €3.5m.(Kicker)

    Witsel:Stoke City imetuma ofa rasmi ya £11m kwenda Zenit St. Petersburg kwa ajili ya kumsajili kiungo fundi wa klabu hiyo Mbelgiji Axel Witsel,26.(The Sun)

    Carrick:Wiki ijayo Michael Carrick atasaini mkataba wa mwaka mmoja wa kuendelea kuitumikia Manchester United.Mkataba wa sasa wa kiungo huyo mwenye umri wa miaka 34 unaisha mwezi ujao lakini kocha Jose Mourinho hataki kuona kiungo huyo wa zamani wa Tottenham anaondoka Old Trafford kipindi hiki.(Sky Sport)

    Bartra:Beki wa Barcelona Marc Bartra,25 amethibitisha kuwa katika mkataba wake kuna kipengele cha kumruhusu kuondoka klabuni hapo kwa dau la £6m.Batra amesema kwasasa sina cha kuongea hatma yangu iko mikononi mwa mwakilishi wangu Carles Puyol.(Mundo)

    Perisic:Chelsea imeripotiwa kutaka kumsajili kiungo wa Inter Milan Mcroatia Ivan Perisic.Inadaiwa Kocha wake Muitaliano Antonio Conte ni shabiki mkubwa wa nyota huyo wa zamani wa Wolfsburg ya Ujerumani.(Gazzetta dello Sport)

    Aubameyang:Borussia Dortmund imekanusha uvumi kuwa imekubali kumuuza mshambuliaji wake hatari Pierre Emerik Aubameyang kwenda Manchester United kwa ada ya £50m.(Mail)


    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Post a Comment

    Item Reviewed: HIZI HAPA HABARI KUBWA ZA USAJILI TOKA BARANI ULAYA JUMAPILI YA LEO MEI 29,2016 Rating: 5 Reviewed By: Unknown
    Scroll to Top