Barcelona,Hispania.
KLABU ya FC Barcelona kupitia kwa Mkurugenzi wake wa Michezo Robert Fernandez imetangaza kuachana na mshambuliaji wake Muhispania Sandro RamÃrez Castillo kufuatia kutoridhishwa na maendeleo yake kikosini.
Sandro,20 mzaliwa wa Las Palmas ameichezea FC Barcelona jumla ya michezo 19 katika kipindi cha misimu miwilili alichofanikiwa kuwa kikosi cha kwanza cha miamba hiyo ya Catalunya.
Katika kipindi hicho chote Sandro amefanikiwa kufungia FC Barcelona mabao wanne,moja katika Ligi ya La Liga na matatu katika michuano ya Copa del Rey dhidi ya CF Villanovense.
Wakati huohuo taarifa nyingine toka FC Barcelona zinasema Muhispania mwingine Marc Batra huenda nae akaonyeshwa mlango wa kutokea kama ilivyokuwa kwa Sandro Ramirez.
0 comments:
Post a Comment