Ng'olo Kante.
Ronaldo:Mshambuliaji wa Real Mreno Madrid Cristiano Ronaldo amesema ni watu wenye wivu tu ndiyo wanaoweza kubeza mafanikio yake ya kuwa Mreno wa Kwanza kushinda ubingwa wa Ulaya mara tatu.(Daily Mail)
Chambers:Kocha wa Arsenal Mfaransa Arsene Wenger anataka kumtoa kwa mkopo mlinzi wake kinda Calum Chambers ili kutoa nafasi kwa klabu hiyo kusajili walinzi wapya.(Telegraph)
Pellegrini:Kocha wa zamani wa Manchester City Mchile Manuel Pellegrini,62, amesema atastaafu kufundisha mpira ikiwa hatapata ofa nzuri katika kipindi hiki cha usajili.(Guardian)
Kante:Kiungo wa Leicester City N'Golo Kante amesisitiza kuwa ana furaha kuwa sehemu ya kikosi cha mabingwa hao wa Ligi Kuu England.Kante,25,amesema nina furaha kuwa hapa [Leceister City],akili yangu inawaza Euro,sisikilizi kile kinachosemwa kwenye vyombo vya habari kwasasa.(L'Equipe)
Lichtsteiner:Mlinzi wa kulia wa Juventus Mswisi Stephan Lichtsteiner ameripotiwa kufikia makubaliano ya mdomo na kocha Antonio Conte kwa ajili ya kuhamia Chelsea hii ni baada ya nafasi yake kuwa mashakani kufuatia Juventus kuwa karibu kumsajili mlinzi Dani Alves kutoka Barcelona.(Emanuele Giulianelli)
Murillo:Arsenal imeripotiwa kuwa katika mbio za kuisaka saini ya mlinzi wa Inter Milan Mcolombia Jeison Murillo,24, lakini itabidi ipambane kwani mlinzi huyo wa zamani wa Malaga anawindwa pia na vilabu vya Leicester City na Stoke City: (Gazzetta dello Sport)
Mata:Barcelona imeripotiwa kuwa itatoa $40m kumsajili kiungo wa Manchester United Mhispania Juan Mata, 28,ikiwa msuguano wake na kocha wa sasa wa klabu hiyo Mreno Jose Mourinho utaendelea. (Mundo Deportivo)
Simeone:Diego Simeone ataendelea kuinoa Atletico
Madrid ikiwa tu mabosi wa klabu hiyo watamuunga mkono katika dirisha lijalo la usajili kwa kumpa fungu kubwa ambalo litamuweza kuwanasa nyota wakali wakali watakaomuwezesha kupambana na vilabu vya Barcelona na Real Madrid.(Mundo Deportivo)
Pickford:Maskauti wa Manchester United wameripotiwa kuifuatilia kwa ukaribu michuano ya vijana ya U-21 ya Toulon tournament kwa lengo la kutazama uwezo wa mlinda mlango wa Sunderland Jordan Pickford, 22. (Chronicle)
Mammana:Chelsea imeripotiwa kuwa katika nafasi nzuri ya kumsajili mlinzi wa River Plate Emanuel Mammana,20, kwa ada ya £8m lakini inakabiriwa na upinzani mkali toka vilabu vya Italia Inter Milan na Fiorentina. (Goal.com)
Campbell:Mlinzi wa zamani wa England Sol Campbell amesema hadhani kama kocha wa timu ya taifa hilo Roy Hodgson kama anaweza kusubutu kumwanzisha John Stones, 22, katika michuano ijayo ya Euro 2016 kwani mlinzi huyo kinda wa Everton amekuwa akifanya makosa mengi.(Evening Standard)
Pereyra: West Ham imetuma ofa ya £11.4m kwenda Juventus kwa ajili ya kumsajili winga Roberto Pereyra, 25,lakini mabingwa hao wa Serie A wanataka £13m. (Tuttosport)
Caulker:Sunderland imeripotiwa kutaka kujiimarisha kwa kumsajili mlinzi wa QPR, Steven Caulker, 24, ambaye anapatikana kwa dau la £4.5m pamoja na mlinzi wa Borussia Dortmund Nevan Subotic, 27, kwa mkopo wa msimu mmoja.(Sunderland Echo)
0 comments:
Post a Comment