Charleroi,Ubelgiji.
KRC Genk inayochezewa na Mshambuliaji wa Kimataifa wa Tanzania Mbwana Ally Samatta amejiweka katika mazingira magumu ya kufuzu michuano ya Europa Ligi msimu ujao baada ya Ijumaa usiku kufungwa kwa mabao 2-0 na Sporting Charleroi huko Stade du Pays de Charleroi.
Katika mchezo huo wa kwanza wa mchujo wa mwisho kuwania nafasi moja iliyobaki ya kufuzu Europa Ligi uliofanyika Uwanja,Samatta aliingia dakika ya 55 akitokea benchi lakini alishindwa kuisaidia KRC Genk kukwepa kichapo hicho.
Mabao ya washindi Sporting Charleroi yamefungwa na Amara Baby dakika ya 43 na Jeremy Perbet dakika ya 50.
Kufuatia matokeo hayo KRC Genk sasa inatakiwa kushinda mabao 3-0 katika
mchezo wake wa marudiano utakaochezwa kesho Jumapili nyumbani Crystal Arena ili iweze kufuzu Europa Ligi.
0 comments:
Post a Comment