Mario Gotze
Dybala:Juventus imeitupilia mbali ofa ya €90m iliyoletwa mezani na Barcelona kwa ajili ya kuitaka saini ya mshambuliaji wake kinda raia wa Argentina Paulo Dybaba,22 na kusisitiza kuwa staa huyo wa zamani wa Palermo hauzwi kwa bei yoyote ile.(Tuttosport)
Sule:Liverpool imeanza kumfukuzia mlinzi kinda wa Hoffenheim Niklas Sule,21 ili kuja kuziba nafasi za walinzi wake wakongwe Kolo Toure na Martin Skrtel wanaotarajia kuondoka hivi karibuni.(The Daily Mail)
Gotze:Mario Gotze,23 amezima uvumi kuwa ataihama Bayern Munich baada ya leo hii kusema kuwa atabakia Allianz Arena ili kupigania namba katika kikosi cha Carlo Ancelloti.Habari hii ni pigo kwa Liverpool iliyokuwa ikimuwania kiungo huyo wa zamani wa Borussia Dortmund.(Bild)
Van Gaal:Manchester United imemlipa Louis van Gaal kitita cha £5m kama fidia ya kuvunja mkataba wake uliokuwa umebakiza miezi 12 ufike mwisho.(BBC Sport)
Mourinho:Kocha mtarajiwa wa Manchester United Mreno Jose Mourinho atapewa kitita cha £200m ili kuwasajili James
Rodriguez,John Stones, Marquinhos, Pierre-Emerick Aubameyang na Zlatan Ibrahimovic.(Daily Mirror)
Benatia:Baada ya kufanikiwa kumsajili kiungo wa Borussia Monchengladbach Granit Xhaka,Arsenal imeripotiwa kurudi tena Ujerumani lakini safari hii ni katika klabu ya Bayern Munich kujaribu kumsajili mlinzi wa kati toka Morocco Mehdi Benatia,29. (Foot Mercato)
Gameiro:Real Madrid imefungua mazungumzo na wakala wa mshambuliaji Sevilla Mfaransa Kevin Gameiro ili kuangalia uwezekana wa kumsajili katika kipindi hiki cha dirisha la usajili.(OK Diario)
Mkhitaryan:Borussia Dortmund imesema kiungo toka Albania Henrikh Mkhitaryan,27 hata ondoka klabuni hapo katika kipindi hiki cha usajili barani Ulaya.(Bild)
Morata:Arsenal imetuma ofa ya £39m kwenda Juventus ikiwa ni jitihada za kutaka kumsajili mshambuliaji wa klabu hiyo Muhispania Alvaro Morata.
Morata,23 ameifungia Juventus mabao 27 katika michezo 93 tangu alipojiunga nayo mwaka 2014 akitokea Real Madrid.(Mundo Deportivo)
Mika:Leicester City imeripotiwa kukubali kutoa kitita cha £1m ili kumsajili mlinda mlango wa Boavista ya Ureno Mika,25.(A Bola)
0 comments:
Post a Comment