728x90 AdSpace

Friday, May 27, 2016

BAADA YA KUONDOKA ARTETA ARSENAL YAPATA NAMBA 8 MPYA


London,England.

KLABU ya Arsenal imetangaza kuwa Kiungo wake Aaron Ramsey ameachana na jezi Na.16 na sasa atakuwa akivaa jezi Na 8 iliyokuwa ikivaliwa na nahodha wake Mikel Arteta anayejiandaa kutua Manchester City kuwa msaidizi wa Kocha Pep Guardiola.

Ramsey,25,amekuwa akivaa jezi Na 16 tangu  alipojiunga na Arsenal mwaka 2008 akitokea Klabu ya Cardiff City ya nyumbani kwao Wales kwa ada ya uhamisho ya £5m.

Akiwa na Cardiff City Ramsey alikuwa akivaa jezi Na.30 na Na. 24.Akiwa na timu yake ya Taifa ya Wales huwa anavaa jezi Na 10.

Ramsey anaingia katika orodha ndefu ya wachezaji wa waliowahi kuvaa jezi namba 8 wakiwa na Arsenal katika vipindi tofauti tofauti.Baadhi ya wachezaji hao ni George Graham, Freddie Ljungberg na Ian Wright.

Wachezaji wengine waliobadilishiwa jezi tayari kwa msimu mpya wa 2016/17 ni Alexis Sanchez ambaye ameachana na jezi namba 17 aliyokuwa akiivaa hapo mwanzo na sasa atakuwa akivaa jezi Na 7 iliyokuwa ikivaliwa na Tomas Rosicky ambaye ameondoka Arsenal.

Mlinda mlango Peter Cech atakuwa akivaa jezi Na.1 badala ya jezi Na.33 aliyokuwa akiivaa hapo awali.

  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

0 comments:

Post a Comment

Item Reviewed: BAADA YA KUONDOKA ARTETA ARSENAL YAPATA NAMBA 8 MPYA Rating: 5 Reviewed By: Unknown