Cairo,Misri.
KILE kitendawili cha timu zipi zitapangwa kundi moja na Mabingwa wa Ligi Kuu Tanzania Bara Yanga SC katika hatua ya nane bora kinakwenda kuteguliwa leo Mei 24,2016.
Taarifa iliyoifikia Soka Extra ni kutoka Shirikisho la Vyama vya Soka Afrika (CAF) ni kwamba droo hiyo itarushwa Live kupitia tovuti rasmi ya Shirikisho hilo ambayo ni,www.cafonline.com .
Droo itafanyika Cairo,Misri yaliko Makao Makuu ya CAF mishale ya saa 12:30 za Misri ambayo ni sawa na saa 13:30 Mchana kwa saa za Tanzania.
Kutoka Ligi ya Mabingwa Timu zilizofuzu ni:
-Al Ahly - Misri
-Zamalek - Misri
-AS Vita - DR Congo
-ASEC Mimosas - Cote d’Ivoire
-ES Setif - Algeria
-Enyimba - Nigeria
-Wydad Athletic Club -Morocco
-Zesco -Zambia
Kutoka Shirikisho Timu zilizofuzu ni:
-Etoile du Sahel - Tunisia ( Mabingwa watetezi)
- Ahly Tripoli - Libya
-MO Bejaia -Algeria
- Medeama -Ghana
- FUS Rabat - Morocco
-Kawkab - Morocco
-TP Mazembe -DR Congo
-Young Africans -Tanzania
0 comments:
Post a Comment