Dar es Salaam,Tanzania
WACHEZAJI wa Klabu Bingwa ya Afrika Mashariki na Kati Azam FC,wamepewa mapumziko ya wiki tano baada ya kumaliza mechi ya mwisho
ya msimu wa 2015/16 dhidi ya Yanga kwenye mchezo wa fainali ya Kombe la
Shirikisho (Azam Sports Federation Cup) juzi jioni.
Akizungumza na mtandao rasmi wa klabu www.azamfc.co.tz Ofisa Mtendaji Mkuu wa Azam FC, Saad Kawemba, alisema kuwa msimu ndio umeisha kwa timu hiyo na kilichobakia ni kujipanga kwa ajili ya kupata matokeo mazuri msimu ujao.
“Tunamshukuru Mwenyezi Mungu tumecheza mchezo wa fainali, ingawa matokeo yalikuwa si mazuri haikuwa
malengo yetu, tulipanga kushinda lakini lazima tukubali ni matokeo ya mpira,” alisema.
Kawemba alisema wachezaji watamaliza likizo hiyo Juni 30 mwaka huu na Julai Mosi wataanza maandalizi ya msimu mpya.
“Kwa hiyo tutafanya nini kwa msimu ujao,tutamuongeza nani, tutamtoa nani hayo tutazungumza baadaye
lakini sasa hivi tunawaomba washabiki wetu wawe watulivu na
tutaendelea kujipanga,” alisema.
0 comments:
Post a Comment