Kigali,Rwanda.
IKIWA katika dimba lake la nyumbani la Amahoro, RWANDA imefungwa mabao 2-0 na Senegal katika mchezo mkali wa kimataifa wa kirafiki uliochezwa Jumamosi jioni jijini Kigali,Rwanda.
Mchezo huo uliokuwa maalumu kwa ajili ya kujiandaa na michezo ya kufuzu michuano ya AFCON ilishuhudiwa wageni Senegal wakipata bao la kuongoza dakika ya 14 tu ya mchezo kupitia kwa mshambuliaji wake Diouf Mame Biram.
Diouf anayechezea Stoke City ya England alifunga bao hilo kwa mkwaju mkali uliomuacha kipa wa Rwanda Eric Ndayishimiye akiwa hana la kufanya.Senegal iliongeza bao la pili dakika ya 30 kupitia kwa Sankhare Younnouse na kuifanya Senegal iende wapumziko ikiwa mbele kwa mabao hayo mawili.
Kipindi cha pili kocha wa Rwanda,Johnny McKinstry aliamua kukifanyia mabadiliko kikosi chake kwa kuwaingiza wachezaji sita,Danny Usengimana,Dominique Savio,Haruna Niyonzima,Michel Rusheshangoga , Ally Niyonzima na Thierry Manzi.
Mabadiliko hayo hayakuzaa matunda zaidi ya kuzuia mabao zaidi toka kwa Senegal iliyokuwa ikitiwa chachu na mbio za winga wake Sadio Mane.
Senegal itashuka tena dimbani Juni 4 huko Bujumbura kuvaana na wenyeji Burundi katika mchezo wa Kundi K wa kuwania kufuzu AFCON,Siku hiyo hiyo Rwanda watakuwa nyumbani Amahoro kuikaribisha Msumbiji katika mchezo wa Kundi H
0 comments:
Post a Comment