728x90 AdSpace

  • Latest News

    Saturday, May 28, 2016

    KUELEKEA COPA CENTENARIO:ARGENTINA YASHINDA,MESSI AUMIA, AKIMBIZWA HOSPITALI

    SAN JUAN,ARGENTINA.

    Lionel Messi amelazimika kukimbizwahospitalli kwa ajili ya kupatiwa matibabu zaidi baada ya kuumia mgongo wakati akiichezea Argentina katika mchezo wa Kimataifa wa Kirafiki dhidi ya Honduras uliomalizika kwa wenyeji Argentina kushinda kwa bao 1-0.


    Katika mchezo huo uliokuwa maalumu kwa ajili ya maandalizi ya michuano ya Copa America Centenario itakayofanyika mwezi ujao nchini Marekani,Messi alitolewa uwanjani dakika ya 64 na nafasi yake kuchukuliwa na Ever Banega baada ya kugongwa na goti mgongoni na mlinzi wa Honduras Maynor Figueroa na kushindwa kuendelea na mchezo kutokana na kupata maumivu makali. 

    Bao pekee la ushindi katika mchezo huo limefungwa na mshamuliaji Gonzalo Higuain dakika ya 31 akiunganisha krosi murua toka kwa mlinzi wa kushoto Marcos Rojo.

    Kabla ya kufunga bao hilo Higuain alimpiga chenga mlinzi wa Honduras Maynor Figueroa na kisha kumfunga kirahisi mlinda mlango Donis Escober.

    Argentina itafungua pazia la michuano ya Copa America Centenario kwa kuvaana na Chile Juni 6 huko California katika uwanja wa Levi,Santa Clara.

    VIKOSI

    Argentina: Sergio Romero; Gabriel Mercado, Nicolás Otamendi, Ramiro Funes Mori, Marcos Rojo; Lucas Biglia, Javier Mascherano, Erik Lamela; Lionel Messi,Gonzalo Higuaín na Angel Di María.

    Honduras: Donis Escober; Brayan Beckeles, Johny Palacios, Maynor Figueroa,Emilio Izaguirre; Jorge Claros, Bryan Acosta,Johnny Leverón, Romel Quioto; Alberth Elis na Marco Tulio Vega.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Post a Comment

    Item Reviewed: KUELEKEA COPA CENTENARIO:ARGENTINA YASHINDA,MESSI AUMIA, AKIMBIZWA HOSPITALI Rating: 5 Reviewed By: Unknown
    Scroll to Top