Munich,Ujerumani.
Klabu ya Bayern Munich imekamilisha usajili wa mlinzi wa kati Mats Hummels kutoka Borussia Dortmund kwa ada ya uhamisho inayokadiriwa kufikia £30m ($45m)
Hummels,27 amesaini mkataba wa miaka mitano.Mkataba huo unatarajiwa kufikia tamati yake hapo Juni 30,2021.
Akiwa na Borussia Dortmind,Hummels alifanikiwa kutwaa mataji mawili ya Bundesliga hii ikiwa ni mwaka 2011 na 2012 pamoja na taji moja la DFB-Pokal mwaka 2012.Mwaka 2013 aliifikisha Borussia Dortmund fainali ya Ligi ya Mabingwa Ulaya na kufungwa na Bayern Munich.
Hummels anakuwa mchezaji wa tatu kujiunga na Bayern Munich akitokea Borussia Dortmund.Wengine ni Mario Goetze na Robert Lewandowski .
Kwa usajili huu ni kama Hummels amerudi nyumbani kwani alianzia soka lake Bayern Munich kabla ya msimu wa 2007/08 kujiunga na Borussia Dortmund.
0 comments:
Post a Comment