Samuel Umtiti
PARIS,UFARANSA.
ZIKIWA zimebaki siku chache michuano ya Euro ianze kutimua vumbi lake nchini Ufaransa,ukuta wa timu ya taifa hilo umeendelea kumomonyoka baada ya jioni hii mlinzi wake Jeremy Mathieu kuondolewa kikosini kutokana na kuwa majeruhi.
Mathieu,30 anayechezea FC Barcelona ameondolewa kikosini baada ya vipimo kuonyesha kuwa bado hajapona vyema majeraha ya misuli yaliyokuwa yanamkabili,nafasi yake imechukuliwa na mlinzi wa Lyon Samuel Umtiti.
Mathieu anakuwa mlinzi wa tatu kuondolewa katika kikosi cha Ufaransa katika kipindi kisichozidi mwezi mmoja.Wengine ni Raphael Varane wa Real Madrid na Mamadou Sakho wa Liverpool.
0 comments:
Post a Comment