728x90 AdSpace

  • Latest News

    Wednesday, May 25, 2016

    NDUGU WASUSIA NDOA YA JAMIE VARDY INAYOFUNGWA LEO JUMATANO

    Leceister ,England.

    SHUJAA wa Leicester City na timu ya taifa ya England Jamie Vardy leo Jumatano atakuwa anafunga ndoa na mpenzi wake wa muda mrefu Mrembo Becky Nicholson huko Peckforton
    Castle,Cheshire.

    Kitu kibaya katika ndoa hiyo ni kwamba wazazi wote wawili wa Vardy,29 baba na mama pamoja na babu na bibi yake hawata hudhuria ndoa hiyo kwa kile kinachodaiwa kuwa hawamtaki bibi harusi mtarajiwa Becky Nicholson. 
    Chanzo chetu cha habari kimepasha kuwa kwa kipindi kirefu sasa Vardy amekuwa katika mgogoro na familia yake kiasi kwamba hajawahi kuongea na wazazi wake kwa kipindi cha miezi 18,hakuna aliyealikwa harusini.

    Familia haimtaki Becky,34 ambaye tayari ameshazaa na Vardy mtoto wake kike aitwaye Sofia mwenye umri wa mwaka mmoja.

    JE,FAMILIA YA VARDY INASEMAJE?? 

    Lisa mama mzazi wa Vardy amesema “Siwezi kusema chochote kile kwa mwanangu,kiwe kibaya au kizuri.Sisumbuki.Naamka naenda zangu kazini narudi nahudumia familia yangu basi.Siendi harusini"

    Phil Vardy,baba wa kambo/mlezi wa Vardy amesema:"Sio vizuri kuongea chochote katika kipindi kama hiki.Lakini mambo yamekuwa hayaendi sawa tangu Vardy ampate Becky.Ni aibu na huzuni.Hakuna tena mahusiano ya moja kwa moja na mwanangu lakini bado mimi ni shabiki wake namba moja"

    Richard Gil,52 baba mzazi wa Vardy:Gil ambaye amefahamu kuwa Vardy ni damu yake miezi mitano tu iliyopita baada ya kumwagana na Lisa miaka mingi iliyopita yeye amesema hana tatizo lolote.

    JE,FAMILIA YA BECKY INASEMAJE?

    Familia ya Becky haina matatizo na Vardy na imesema imefurahi kupata mototo wa kiume katika familia hiyo yenye mabinti watupu wanne.

    Ndoa ya Vardy na Becky itafungiwa katika hekalu la Peckforton huko Cheshire.Hekalu hilo hutumika kufungia ndoa nyingi za mastaa wa soka nchini England.

    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Post a Comment

    Item Reviewed: NDUGU WASUSIA NDOA YA JAMIE VARDY INAYOFUNGWA LEO JUMATANO Rating: 5 Reviewed By: Unknown
    Scroll to Top