London,England.
BAADA ya habari kuvuja kuwa mlinzi wa Kimataifa wa Ufaransa Laurent Koscielny,30 ndiye atakayekuwa nahodha mpya wa Arsenal akichukua nafasi ya Mikel Arteta aliyeondoka,mashabiki wa klabu hiyo kwa nyakati tofauti wamepinga mlinzi huyo wa zamani wa Lorient kupewa jukumu hilo kwa madai kuwa siyo kiongozi.
Mashabiki hao wakitumia mitandao ya kijamii kutoa mawazo yao juu ya mchezaji yupi hasa anayefaa kuchukua nafasi ya Arteta asilimia kuwa wameonyesha kutokuwa na imani na Koscielny ambaye amekuwa na klabu hiyo tangu mwaka 2005.
Licha ya kukiri kuwa Mfaransa huyo ni nguzo katika safu ya ulinzi ya klabu yao,mashabiki hao wamesema Koscielny hana sifa za kuwa nahodha,siyo kiongozi na hana maamuzi ya moja kwa moja na badala yake wamependekeza jukumu hilo apewe Peter Cech ama Jack Wilshere.
Mapema wiki hii kuliibuka habari kuwa Kocha wa Arsenal Arsene Wenger anataka kumpa cheo cha unahodha Koscielny kama zawadi baada ya mwanzoni mwa msimu uliopita kukataa kujiunga na Bayern Munich licha ya Klabu hiyo ya Ujerumani kuja na ofa nono.
Kama habari hizo zitakuwa ni kweli basi Koscielny atakuwa Mfaransa wanne kuwa nahodha wa Arsenal baada ya Patrick Vieira, Thiery Henry na William Gallas.
0 comments:
Post a Comment