728x90 AdSpace

  • Latest News

    Saturday, May 28, 2016

    HIZI HAPA HABARI KUBWA ZA USAJILI TOKA PANDE ZOTE ZA DUNIA JUMAMOSI YA LEO MEI 28,2016.

    Ricardo Rodriguez

    Yondani:Klabu ya Yanga SC imewaongezea mikataba mipya ya miaka miwili kila mmoja nyota wake Kelvin Yondani,Oscar Joshua na Ally Mustafa "Barthez".Mikataba hiyo itafikia tamati mwaka 2018.

    Zouma:Kocha wa Arsenal Arsene Wenger ameripotiwa kuwa amefanya mawasiliano na kocha wa Chelsea Antonio Conte ili kuangalia uwezekano wa kumsajili mlinzi wa klabu hiyo Mfaransa Kurt Zouma,21.(Daily Mail)

    Ranieri:Kocha Muitaliano Claudio Ranieri anakaribia kukubali kusaini mkataba mpya wa miaka mitatu wa kuendelea kuinoa Leceister City.Mkataba huo mpya utamuwezwesha Ranieri kuvuna mshahara wa £3m kwa mwaka ambao ni mara mbili zaidi ya ule wa sasa wa £1.5m.(Daily Telegraph)

    Oscar:Kocha wa Chelsea Muitaliano Antonio Conte amesema kuwa atapambana kwa nguvu zake zote kuhakikisha winga wake Willian da Silva haendi klabu yoyote ile ikiwemo Manchester United lakini amesisitiza kuwa klabu inayomtaka kiungo wake Oscar Dos Santos ije kwani nyota huyo anauzwa.(Daily Mail)

    Ozil:Arsenal inahofia kuwa Bayern Munich imeanza kumfukuzia kiungo wake Mjerumani Mesut Ozil.Hofu hiyo imekuja baada ya Ozil,27,kukataa kwa mara ya pili kujongea katika meza ya mazungumzo kwa ajili ya mkataba mpya.(The Sun)

    Rodriguez:Arsenal imeonyesha nia ya kutaka kuimarisha safu yake ya ulinzi hasa ulinzi wa kushoto baada ya kuripotiwa kuvutiwa na huduma ya mlinzi wa kushoto wa Wolfsburg,Mswisi Ricardo Rodriguez,24 na huenda ikamtwaa kwa ada ya £19m.(Kicker)

    Ibrahimovic:Wakala wa mshambuliaji Zlatan Ibrahimovic,anayeitwa Mino Raiola amesema mteja wake bado hajaamua wapi atakwenda na taarifa kuwa anaelekea Manchester United ni uzushi mtupu.Amesema "Kila mtu anaongea kuhusu Man United,hii ndiyo sababu huwa siongea mara kwa mara na waandishi wa habari.(Sky/Expressen)

    Zapata:Arsenal imeripotiwa kutaka kumsajili mshambuliaji wa Napoli anayecheza kwa mkopo Udinese Mcolombia Duvan Zapata.Zapata,25 ameifungia Udinese mabao manane katika michezo 25.
    Udinese's president Franco Soldati.(Radio Kiss Kiss)

    Lewandowski:Mwenyekiti Mtendaji wa Bayern Munich Karl-Heinz Rummenigge amesema hawezi kukaa mezani na Uongozi wa Real Madrid kufanya mazungumzo ya kumuuza mshambuliaji wake Robert Lewandowski.Rummenigge amesisitiza kuwa Lewandowski,27 hauzwi kwa bei yoyote ile.(Kicker)

    Krychowiak:Kiungo wa Sevilla anayewindwa na Manchester United, Mpoland Grzegorz Krychowiak amemwambia wakala wake asisikilize ofa yoyote ile itakayoletwa kwa ajili yake kwani hana mpango wa kuhama Ramon Sanchez Pizjuan msimu huu.(Macca)

    Vidal:Barcelona imeiambia Liverpool kama inataka kumsajili mlinzi wake wa kulia Aleix Vidal basi iandae kitita cha £45m.(Mundo Deportivo)


    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Post a Comment

    Item Reviewed: HIZI HAPA HABARI KUBWA ZA USAJILI TOKA PANDE ZOTE ZA DUNIA JUMAMOSI YA LEO MEI 28,2016. Rating: 5 Reviewed By: Unknown
    Scroll to Top