Johannesburg, Afrika Kusini.
KOCHA wa zamani wa Bafana Bafana na vilabu vya Orlando Pirates,Kaizer Chiefs na Mamelodi Sundowns Ted Dumitru,76 amefariki dunia leo mchana huko Johannesburg,Afrika Kusini kwa ugonjwa wa moyo.
Kwa mujibu wa vyanzo mbalimbali vya habari vya Afrika Kusini ni kwamba Dumitru alidondoka wakati akifanya manunuzi (Shopping) katika kituo cha biashara cha Eastgate Mall na kukimbizwa hospitali ambako baada ya muda mfupi alitangazwa amefariki.
Kabla ya kifo chake Dumitru aliiviwezesha vilabu vya Kaizer Chiefs na Mamelodi Sundowns kutwaa ubingwa wa Ligi Kuu wa Afrika Kusini mara mbili kila kimoja.
Aliiwezesha Mamelodi Sundowns kutwaa ubingwa wa Ligi Kuu mwaka 1998 na 1999 kisha Kaizer Chiefs mwaka 2004 na 2005.Pia aliiongoza Bafana Bafana kufuzu michuano ya AFCON iliyofanyika nchini Misri mwaka 2016 na kutolewa katika hatua ya makundi
0 comments:
Post a Comment