Genk,Ubelgiji.
NDOTO ya Mshambuliaji wa Kimataifa wa Tanzania Mbwana Samatta kucheza michuano ya Europa Ligi msimu ujao imetimia baada ya jioni ya leo klabu yake ya KRC Genk kufuzu hatua ya mtoano kufuatia kuifunga Charleroi kwa mabao 5-1 katika mchezo mkali wa marudiano uliochezwa katika uwanja wa Cristal Arena.
Mabao yaliyoipa ushindi huo mnono KRC Genk yamefungwa na Nikos Karelis aliyefunga mabao matatu (20,56,71),Mbwana Samatta (27) na Sandy Walsh (45).Bao la kufutia machozi la Charleroi limefungwa dakika ya 40 na Jeremy Perbet.
Dakika ya 16 na Charleroi ilipata pigo baada wachezaji wake wawili Nikolas Pennetaeu na Baby kulimwa kadi nyekundu na kulazimika kumaliza mchezo ikiwa na wachezaji tisa.
Kwa matokeo hayo KRC Genk imeshindwa kwa jumla ya mabao 5-3.Katika mchezo wa kwanza Charleroi ilishinda kwa mabao 2-0.
0 comments:
Post a Comment