Geneva,Uswisi.
Ubelgiji imetoka nyuma na kuifunga Uswisi kwa mabao 2-1 katika mchezo wa kimataifa wa kirafiki uliochezwa Geneva,Uswisi jioni ya leo.
Wenyeji Uswisi ndiyo walikuwa wa kwanza kupata bao dakika ya 31 kupitia kwa Blerim Dzemaili .Dakika ya 34 Romero Lukaku aliisawazishia bao Ubelgiji kabla ya dakika ya 83 Kevin De Bruyne kufunga bao la ushindi.
Dakika 81 Uswisi ilipata pigo baada ya mlinzi wake Haris Seferovic kulimwa kadi nyekundu kwa mchezo mbaya.
KIKOSI
Belgium: Courtois, Witsel, Alderweireld,Vermaelen, Vertonghen, Fellaini, Dembele, De Bruyne, Mertens, E Hazard, R Lukaku
0 comments:
Post a Comment