Liverpool, England.
Liverpool imemsajili mlinda mlango Loris Karius toka Mainz ya Ujerumani kwa ada ya £4.7m.
Karius,22 ambaye aliwahi kunolewa katika shule ya soka ya Manchester City kuanzia mwaka 2009 mpaka 2011 amesaini mkataba wa miaka mitano na kukabidhiwa jezi namba 1.
Karius anakuwa mchezaji wa tatu kujiunga na Liverpool tangu Mjerumani Jurgen Klopp apewe kibarua cha kuinoa miaka hiyo ya Anfield.Wengine ni Joel Matip toka Cameroon na Marko Grujic toka Serbia.
Liverpool imeamua kumsajili Karius ili kumpa changamoto mlinda mlango wake namba Moja Mbelgiji Simon Mignolet ambaye amekuwa akifanya makosa mengi langoni.
0 comments:
Post a Comment