728x90 AdSpace

  • Latest News

    Friday, May 27, 2016

    AZAM YATOA BILIONI MBILI KUDHAMINI LIGI YA WANAWAKE,VIJANA

    Dar es Salaam,Tanzania.

    KAMPUNI ya Azam Media Limited na Shirikisho la Soka Tanzania TFF leo kwa pamoja wameandika historia mpya katika soka la Tanzania baada ya kusaini mkataba wa miaka mitano wenye thamani ya Sh. bilioni mbili kwa ajili ya kuzidhamini Ligi Kuu ya Wanawake na ile ya Vijana wa umri wa chini ya miaka 20.

    Udhamini huo ambao umetiwa saini katika Ofisi za Azam Media Limited zilizoko Tazara jijini Dar es Salaam umejumuisha pia kurushwa Live kupitia runinga kwa michezo yote ya Ligi hizo.

    Akizungumza baada ya kukamilisha mchakato wa utiwaji saini wa mkataba huo Mtendaji wake Mkuu wa Azam Media Limited Rhys Torrington amesema lengo la Kampuni yake ni kuhakikisha mpira wa Tanzania unapiga hatua kubwa kimaendeleo.

    Rais wa TFF Jamal Malinzi
    yeye ameupongeza Uongozi wa Azam Media Limited kwa kuamua kuzinyanyua Ligi za Wanawake na Vijana ambazo kwa kipindi kirefu zimekuwa zikikosa udhamani.

    Ligi ya wanawake ambayo itaanza Agosti mwaka huu na itashirikisha jumla ya timu 10. 

    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Post a Comment

    Item Reviewed: AZAM YATOA BILIONI MBILI KUDHAMINI LIGI YA WANAWAKE,VIJANA Rating: 5 Reviewed By: Unknown
    Scroll to Top