London, England.
MARCUS RASHFORD,18, amejumuishwa katika kikosi cha mwisho cha wachezaji 23 kitakachoiwakilisha England katika michuano ya Ulaya inayotarajiwa kuanza Juni 10 huko Ufaransa.
Wakati Rashford akipenya katika kikosi hicho cha kocha Roy Hodgson,winga wa Newcastle United Andros Townsend,Kiungo wa Leicester City Danny Drinkwater na Kiungo wa Manchester City Fabian Delph wao wametemwa.
England itaianza michuano ya Euro kwa kucheza na Urusi Juni 13.
KIKOSI KAMILI
Makipa: Hart, Forster, Heaton
Mabeki: Walker, Rose, Cahill, Smalling,Clyne, Stones, Bertrand
Viungo: Milner, Sterling, Lallana,Henderson, Dier, Wilshere, Barkley, Alli
Washambuliaji: Kane, Rooney, Vardy, Sturridge,Rashford
0 comments:
Post a Comment