728x90 AdSpace

  • Latest News

    Tuesday, May 31, 2016

    KIPRE TCHETCHE AIRUKA YANGA SC MITA 100%

    Dar es Salaam,Tanzania.

    MSHAMBULIAJI wa Azam FC, Kipre Tchetche inayedaiwa amesaini kuichezea klabu ya Al-Nahda Al-Buraimi ya Oman, amesema bado ana mkataba na Azam ingawa kwa sasa kiu yake ni kucheza soka nje ya mipaka ya Tanzania.

    Amesema anapanga kukutana na uongozi wa klabu hiyo umruhusu kuondoka, kwani ameshaamua kuachana na soka ya Tanzania,hivyo asihusishwe na klabu yoyote,ikiwemo Yanga.

    Hivi karibuni, kiongozi mmoja wa Al Nahda inayoshiriki Ligi Kuu ya Oman, alituma kwenye akaunti yake ya Twitter picha za Kipre Tchetche akisaini mikataba na kuandikia; “M-ivory Coast Kipre Tchetche rasmi mchezaji wa kwanza wa kigeni Al Nahda.”

    Katika picha hizo, Kipre anaonekana akisaini mikataba hiyo akiwa nyumbani kwake, Kijichi, Dar es Salaam katika nyumba aliyopangiwa na Azam.

    Pamoja na hayo, Kipre mwenyewe amekana kusaini timu yoyote,akisema ameshaamua kuachana na soka ya Tanzania na kwamba kiu yake ni kwenda kupata changamoto nyingine nchi nyingine.

    Akizungumza jana kutoka kwao Ivory Coast, ambako yuko kwa mapumziko, Kipre alisema anataka kuzungumza na uongozi wa Azam imruhusu aondoke.

    “Inatosha kwa muda ambao nimecheza Tanzania, nahitaji kuondoka kwenda kutafuta changamoto nyingine kwingine.

    Nimekuwa na maisha mazuri sana Azam, viongozi na wamiliki wanajali sana wachezaji, lakini nalazimika kuyaacha yote,” alisema mchezaji huyo aliyebakiza mwaka mmoja katika mkataba wake wa kuichezea Azam.

    Na inadaiwa kuwa tayari Azam imeambatanisha picha za Kipre Tchetche na barua ya malalamiko kupeleka Shirikisho la Kimataifa la Soka (FIFA) ikiishitaki Al Nahda na mchezaji mwenyewe. Awali, ilidaiwa Kipre yuko mbioni kutua Yanga na tayari ameandaliwa dau la Sh milioni 180 aweze kujiunga na mabingwa hao wa Tanzania Bara.

    “Nitoke Azam, niende Yanga? Usinifanye nicheke…mimi nimesema sitaki kuendelea kucheza Tanzania na hadi sasa sijasaini kokote hadi nipewe ruhusa na uongozi wa Azam,” alikaririwa na mtandao moja wa hapa nchini.

    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Post a Comment

    Item Reviewed: KIPRE TCHETCHE AIRUKA YANGA SC MITA 100% Rating: 5 Reviewed By: Unknown
    Scroll to Top