Manchester, England.
Licha ya kuipa kombe la FA Jumamosi jioni,Manchester United imetangaza kumtimua Kazi aliyekuwa kocha wake Mkuu Mholanzi Louis van Gaal.
Habari za ndani zinasema Mwenyeki Mtendaji wa Manchester United Ed Woodward asubuhi ya leo alifika katika uwanja wa mazoezi wa klabu hiyo wa Carrington na kufanya mazungumzo mazito na kocha huyo mwenye miaka 64 kabla ya kutangaza kumtimua.
Mbali ya Van Gaal pia wasaidizi wake Frans Hoek, Albert Stuivenberg na Max
Reckers nao wametupiwa virago.Hatma ya Ryan Giggs bado haijulikani.
Hatua hiyo ya kumtimua Van Gaal imefikiwa baada kuwepo kwa shinikizo la muda mrefu kutoka kwa mashabiki na wachezaji wa zamani wa klabu hiyo kutaka kocha huyo atimuliwe kutokana na kushindwa kuirudisha Manchester United kuipa klabu hiyo mafanikio makubwa.
Wakati huohuo habari kutoka Manchester United zinadai kuwa Jose Mourinho huenda akatangwa wiki hii kuwa kocha wa miamba hiyo ya Old Trafford.
0 comments:
Post a Comment