KIUNGO wa Licester City Mfaransa N'Golo Kante amegomea mkataba mpya aliyopewa na Mabingwa hao wa Ligi Kuu England katika kile kinachodaiwa kuwa ni kuilazimisha klabu hiyo kusikiliza ofa toka vilabu vya Arsenal, Chelsea na Paris Saint Germain ambavyo katika siku za hivi karibuni vimedaiwa kuisaka saini yake kwa nguvu zote.
Habari kutoka mtandao wa Le Parisien wa Ufaransa zinadai Kante,25 mwenye kipengele cha kuuzwa kwa £25m anataka kuihama Leceister City katika majira haya ya usajili licha ya kuitumikia kwa msimu mmoja tu klabu hiyo ya King Power iliyomsajili mwezi Augusti mwaka jana kwa ada ya £7m toka Caen.
Kwa mujibu wa chanzo cha habari kinachodaiwa kuwa karibu zaidi na kiungo huyo zinadai Kante ataondoka Leceister City lakini atabakia Ligi Kuu England.Hana mpango wa kurejea Ufaransa licha Paris Saint Germain kumtengea maslahi mazuri zaidi kuliko vilabu vingine vinavyomuwania.
0 comments:
Post a Comment