728x90 AdSpace

  • Latest News

    Monday, May 23, 2016

    KUELEKEA MCHEZO DHIDI YA TAIFA STARS,MITIHANI YAMUONDOA MMOJA KIKOSI CHA MAFARAO

    Cairo,Misri.

    Misri itazikosa huduma za mshambuliaji wake kinda Ramadan Sobhi,18 pale itakapokuja Tanzania Juni 4 kuvaana na Taifa Stars katika mchezo wa marudiano wa kusaka tiketi ya kufuzu michuano AFCON itakayofanyika nchini Gabon mwakani.

    Kwa mujibu wa Mkurugenzi wa Timu ya Taifa ya Misri Ihab Lehta ni kuwa nyota huyo hatafika kutokana na kukabiriwa na mitihani.Bado ni mwanafunzi.

    Lehta amesema "Ramadan Sobhi hatacheza mchezo wetu dhidi ya Tanzania kwa sababu anapaswa kubaki Misri kwa ajili ya kufanya mitihani yake ya High School.

    "Mchezo utakuwa Juni 4, mitihani yake itakuwa Juni 5.Tunasikitika, tumeshindwa kupata ndege ya moja kwa moja ambayo ingeweza kumsafirisha kurudi Misri kuwahi mitihani baada ya mchezo.Hivyo hatakuwa sehemu ya kikosi kitakachokwenda Tanzania.

     "Hilo ni pigo kubwa kwetu.Ramadan ni mmoja kati ya wachezaji wetu muhimu mno lakini tunapaswa kuwaamini waliobakia pia.Alimaliza Lehta.

    Sobhi anayeichezea pia klabu ya Al Ahly ndiye aliyeifungia Misri bao la ushindi dhidi ya Nigeria huko Alexandria na ndiye aliyetoa pasi kwa Mohamed Salah katika mchezo wa kwanza ambao Misri ilitoka sare ya bao 1-1 na Nigeria huko Kaduna,Nigeria.

    Misri itavaana na Taifa Stars Juni 4 katika uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam ambapo ushindi au sare yoyote ile utaifanya miamba hiyo ya Afrika Kaskazini ifuzu fainali za Gabon hapo 2017.


    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Post a Comment

    Item Reviewed: KUELEKEA MCHEZO DHIDI YA TAIFA STARS,MITIHANI YAMUONDOA MMOJA KIKOSI CHA MAFARAO Rating: 5 Reviewed By: Unknown
    Scroll to Top