Sergio Busquets.
Busquets:Sergio Busquets amesaini mkataba mpya wa miaka mitano wa kuendelea kuichezea FC Barcelona.Mkataba huo mpya utakaofikia tamati mwaka 2021umedaiwa kuwa na kipengele ambacho kitamruhusu Busquets,27 kuhama ikiwa klabu itakayotaka kumsajili itakubali kutoa kitita cha €200m.(Mundo Deportivo)
Niguez:Kocha mpya wa Manchester United Jose Mourinho ameripotiwa kuwa yuko tayari kutoa kitita cha £54m pamoja na mshahara mnono ili kumsajili kiungo kinda wa Atletico Madrid Saul Niguez.(The Independent)
Holding:Arsenal imeongeza ofa yake mpaka kufikia £1.2m kwa ajili ya kumsajili mlinzi kinda wa Bolton Wanderers Rob Holding,20,baada ya ile ya awali ya £750,000 kukataliwa.Hata hivyo ofa hiyo mpya inatarajiwa kukataliwa kwani Bolton Wanderers inataka £4m ili iweze kumuachia mlinzi huyo aliyebakiza miezi 12 katika mkataba wake.(Daily Mail)
Zouma:AS Roma imeripotiwa kuwa itafikiria kuwasajili walinzi Kurt Zouma,21wa Chelsea ama Samuel Umtiti wa Lyon ikiwa mlinzi wake Mjerumani,Antonio Rudiger ataondoka Estadio Olympico.(Gazzetta dello Sport)
Koulibaly:Napoli imekataa ofa ya £30m toka kwa Mabingwa wa Bundesliga Bayern Munich kwa ajili ya kumuuza mlinzi wake wa kati Msenegal Kalidou
Koulibaly,25,anayewaniwa pia na vilabu vya Arsenal,Chelsea na Manchester United.(Express)
Guardiola:Meneja mpya wa Manchester Muhispania Pep Guardiola anataka kusajili wachezaji wapya wanane kwa ajili ya kukipa makali kikosi hicho ambacho msimu huu kimeshika nafasi ya tatu Ligi Kuu England.(Daily Mirror)
Stam:Mlinzi wa zamani wa Manchester United Mholanzi Jaap Stam anawindwa na Reading ili kuchukua nafasi ya kocha Brian McDermott aliyetimuliwa Kazi leo hii. Kwa sasa Stam,43 anahudumu katika klabu ya Ajax kama kocha msaidizi.
Ramos:Kocha wa zamani wa Tottenham Juande Ramos ametangazwa kuwa kocha mpya wa Malaga baada ya kusaini mkataba wa miaka mitatu.Ramos amekuwa hana Kazi tangu alipoachana na Dnipro Dnipropetrovsk mwaka 2014.(Goal.Com)
0 comments:
Post a Comment