Dar es Salaam,Tanzania.
SIMBA imeepusha ugomvi kwa kumalizana na aliyekuwa beki wake, Donald Mosoti kwa kumlipa fedha zake Sh. 62.8 Milioni kama ilivyoagizwa na Fifa.
Fifa ilitishia kuishusha daraja Simba na kuifungia Tanzania kushiriki michuano ya kimataifa baada ya klabu hiyo kupuuza agizo la kuitaka imlipe Mosoti kiasi cha Sh 64 Milioni kwa kuvunja mkataba wake na malimbikizo mengine ya fedha za usajili.
Mosoti jana Ijumaa alilithibitisha kuwa, ameshalipwa chake tangu Jumanne iliyopita, japo nyaraka zinaonyesha Simba iliingiza fedha Mei 19, 2016. “Nashukuru Simba imenilipa changu, siwadai, hawanidai,”alisema Mkenya huyo.
0 comments:
Post a Comment