Basel,Uswisi.
KOCHA wa timu ya Taifa ya Ujerumani Joachim Low leo mchana ametangaza kikosi chake cha mwisho cha wachezaji 23 kitakachosafiri kwenda nchini Ufaransa kuiwakilisha nchi hiyo katika michuano ya Ulaya (Euro 2016) inayotarajiwa kuanza kutimua vumbi lake Juni 10.
Katika kikosi hicho kilichoweka kambi nchini Uswisi Law amemwacha winga wa Borussia Dortmund Marco Reus kutokana na kuwa majeruhi.
Akizungumzia uamuzi wa kumwacha Reus,Law amesema "Reus ni mgonjwa anaweza kukimbia tu,hawezi kugeuka kwa kasi.Inauma kumwacha mchezaji kama Reus lakini hatuna jinsi imebidi"
Wengine waliotemwa katika kikosi hicho ni mshambuliaji Karim Bellarabi,Julian Brandt wote kutoka Bayer Leverkusen na Sebastian Rudy wa 1899 Hoffenheim.Mkongwe Bastian Schweinsteiger yeye amejumuishwa licha ya kutokuwa kamili kiafya.
Hii ni mara ya pili kwa Reus kukosa michuano mikubwa mara ya kwanza ni mwaka 2014 alipokosa fainali za kombe la dunia na Ujerumani kuibuka kidedea kwa kuifunga Argentina kwa bao 1-0.
KIKOSI KAMILI
Makipa: Manuel Neuer (Bayern Munich),
Bernd Leno (Bayer Leverkusen), Marc-Andre ter Stegen (Barcelona)
Mabeki: Jerome Boateng (Bayern Munich), Emre Can (Liverpool), Jonas Hector (Cologne), Benedikt Howedes (Schalke), Mats Hummels (Borussia Dortmund), Shkodran Mustafi (Valencia),
Antonio Rudiger (Roma)
Viungo: Julian Draxler (Wolfsburg),Mario Gotze (Bayern Munich), Sami Khedira (Juventus), Joshua Kimmich (Bayern Munich), Toni Kroos (Real Madrid), Mesut Ozil (Arsenal), Leroy Sane (Schalke), Bastian
Schweinsteiger (Manchester United), Julian Weigl (Borussia Dortmund)
Washambuliaji: Mario Gomez (Besiktas), Thomas Muller (Bayern Munich), Lukas Podolski (Galatasaray), Andre Schurrle (Wolfsburg)
0 comments:
Post a Comment