728x90 AdSpace

  • Latest News

    Monday, May 23, 2016

    ENGLAND KUMKOSA JAMIE VARDY MCHEZO DHIDI YA AUSTRALIA SIKU YA IJUMAA

    London,England.

    Mshambuliaji Jamie Vardy,29 hatakuwa sehemu ya kikosi cha England kitakachoshuka katika dimba la Stadium of Light siku ya Ijumaa jioni kuvaana na Australia katika mchezo wa Kimataifa wa Kirafiki ambao ni maalumu kwa ajili ya kujiweka sawa tayari kwa michuano ya Ulaya (Euro 2016) itakayotimua vumbi lake nchini Ufaransa kuanzia Juni 10.

    Akiongea na wanahabari Kocha Mkuu wa England Roy Hodgson amesema amempa mapumziko mshambuliaji huyo wa Leceister City kwa ajili ya kufanya maandalizi ya ndoa yake anayotarajia kuifunga siku ya Jumatano.

    Amesema "Vardy hatakuwepo katika mchezo wetu wa siku ya Ijumaa kwa sababu siku ya Jumatano atakuwa anafunga ndoa.Nimempa mapumziko kidogo.

    "Kukosekana kwake ni bahati mbaya kwetu,lakini inapaswa ikumbukwe kuwa katikati ya mwaka jana ndoa yake ilipangwa kufanyika mwezi Juni lakini baada ya kumuita kikosini ilibidi aiahirishe.

    Nafikiri huu ni muda muafaka kwake kupata siku mbili tatu za kupumzika,kufanya maandilizi na hatimaye afunge ndoa.

    Wakati Vard akikosekana wachezaji wa Manchester United na Liverpool waliokuwa na majukumu katika vilabu vyao wao wameripotiwa kuwa watakuwa wamejiunga na kikosi cha England na watashuka dimbani siku ya Ijumaa kuivaa Australia.

    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Post a Comment

    Item Reviewed: ENGLAND KUMKOSA JAMIE VARDY MCHEZO DHIDI YA AUSTRALIA SIKU YA IJUMAA Rating: 5 Reviewed By: Unknown
    Scroll to Top