Barcelona,Hispania.
Barcelona imetwaa kwa mara ya pili mfululizo ubingwa wa Kombe la Mfalme wa Hispania maarufu kama Copa Del Rey baada ya Jumapili usiku kuifunga Sevilla kwa mabao 2-0 katika mchezo mkali wa fainali uliochezwa katika uwanja wa Vicente Calderon jijini Madrid.
Katika mchezo huo ulioshuhudia mwamuzi Carlos del Cerro Grande akimwaga kadi 12 za njano na 3 nyekundu zilizokwenda kwa Javier
Mascherano (Barcelona 36), Ever Banega (Sevilla 90) na Daniel Carrico (Sevilla ) zilikuwa ni pasi mbili murua za mchezaji bora wa dunia Lionel Messi ndizo zilizoipa Barcelona ubingwa wa 18 wa Copa Del Rey mbele ya mabingwa wa Europa Ligi Sevilla.
Pasi ya kwanza ya Messi ilimfikia mlinzi wa kushoto Jordi Alba dakika ya 97 na kufunga bao la kwanza kisha pasi ya pili kwa Neymar Dos Santos Jr dakika ya 120 na kupachika bao la pili na la mwisho katika mchezo huo wa kuhitimisha msimu wa 2015/16.
Kufuatia ubingwa huo Barcelona imekuwa ndiyo klabu pekee iliyoutwaa ubingwa huo mara nyingi zaidi ya vilabu vyote vya Hispania.
0 comments:
Post a Comment