Marcos Rashford
London,England.
Nyota wa zamani wa Arsenal,Mfaransa Thierry Henry amemtaka kocha mpya wa Manchester United Mreno Jose Mourinho kutopuuza kiwango cha mshambuliaji kinda wa Klabu hiyo Muingereza Marcus Rashford,18 na badala yake ahakikishe anampa nafasi ya kucheza mara kwa mara.
Henry ambaye kwa sasa anajishughulisha na kazi ya uchambuzi wa masuala ya soka ametoa ushauri huo mapema kufuatia kocha huyo wa zamani wa vilabu vya FC Porto,Chelsea,Inter Milan na Real Madrid kutokuwa na tabia ya kuwaamini/kuwatumia wachezaji wenye umri mdogo kama Marcus Rashford.
Akiongea na Sky Sports,Herry amesema "Kiwango alichokionyesha Marcus Rashford msimu uliopita siyo cha kupuuza hata kidogo.Timothy Fosu-Mensah, vile vile ,siwezi kutaja wote.Mourinho anapaswa kuwatumia vijana hawa kama ambavyo mtangulizi wake Louis Van Gaal amekuwa akifanya.
"Kwa sasa Rashford yuko katika kiwango ambacho hapaswi kupuuzwa na badala yake anatakiwa kupewa malezi na uangalizi ambao utamfanya awe bora zaidi ya alivyo leo.Hata kama Mourinho atafanya usajili wa kutisha lakini anapaswa kuhakikisha Rashford na wenzie wanapata nafasi ya kuonyesha vipaji vyao.
0 comments:
Post a Comment