ST. GALLEN, USWISI.
HISPANIA imeanza vyema maandalizi yake ya kujiwinda na michuano ya Ulaya [Euro 2016] baada ya usiku wa leo kuifunga Bosnia-Herzegovina kwa mabao 3-1 katika mchezo mkali wa kimataifa wa kirafiki uliochezwa huko AFG Arena,St.Gallen-Uswisi.
Shujaa wa Hispania katika mchezo wa leo alikuwa ni Manuel "Nolito" Agudo aliyefunga mabao wawili dakika za 11 na 18,Jingine limefungwa Pedro Rodriguez dakika ya 90.
Bao la Kufutia machozi la Bosnia-Herzegovina limefungwa na Emir Spahic dakika ya 28 ambaye dakika ya 45 Alitolewa nje kwa kadi nyekundu kwa mchezo mbaya.
VIKOSI
Spain: Asenjo; Bellerin, San Jose (Fornals 83),Bartra, Azpilicueta; Cesc (Llorente 60), Bruno;Silva (Denis 46), Asensio (Williams 60), Nolito (Oyarzabal 60); Aduriz (Pedro 46)
Bosnia-Herzegovina : Begovic; Vranjes
(Memisevic 90), Spahic, Kolasinac, Zukanovic;Visca (Hajrovic 46), Besic, Pjanic, Hadzic (Medunjanin 67); Hodzic (Duljevic 57), Dzeko (Djuric 21, Grahovac 78)
Katika mchezo mwingine uliopigwa huko AUGSBURG,Wenyeji Ujerumani wamekiona cha moto baada ya kuchapwa mabao 3-1 na Slovakia kupitia kwa Marek Hamsik,Michal Duris na Juraj Kucka.Bao la Ujerumani limefungwa na Mario Gomez.
0 comments:
Post a Comment