Mbeya,Tanzania.
KLABU ya Mbeya City inayomilikiwa na
Halmashauri ya Jiji la Mbeya,imeshitakiwa TFF na beki wao Erick Mawalla kwa kushindwa kumlipa pesa yake ya usajili na mishahara yake ambayo jumla ni Sh 11 milioni.
Mawalla amedai kuondolewa kikosini hapo tangu mwaka jana na aliambiwa kuwa aliyekuwa kocha wao Meja Abdul Mingange hakuwa na mipango naye.
“Katibu (Emmanuel Kimbe) ndiye aliyenipigia simu kuwa sihitajiki kwenye timu, kocha hakuwa na mpango na mimi, niliomba nipewe barua lakini hakunipa zaidi ya kuniambia nitafute timu nyingine, kikubwa hata mshahara wangu nimeingiziwa kwa mara ya mwisho Oktoba mwaka jana. Hivyo nadai pesa
ya usajili na mishahara tangu kipindi hicho.
“Niliwaandikia barua ambayo niliwapa siku 14 ili wanifafanulie juu ya mambo yangu pamoja na kunilipa haki zangu lakini sijajibiwa,nimekuwa nikipiga simu lakini hazipokelewi ndiyo maana nimeona kimbilio pekee ni TFF ambao watanisaidia namna ya kupata haki
yangu.
Nimepelekea barua jana (juzi) pale TFF siku ambayo muda wa barua ya siku 14 niliyowaandikia Mbeya City ulikuwa unamalizika, nimeishi katika mazingira magumu tangu kipindi hicho,” alisema Mawalla.
Kwa upande wa Kimbe alipoulizwa alisema: “Ni kweli ila suala lake tutalijadili hivi karibuni wakati tunajadili wachezaji watakaoachwa na watakaobaki.Tumepata taarifa juu ya barua hiyo pia,hatukumtumia sana kwasababu aliumia tulipomsajili tu na alicheza mechi moja,tulimuuguza kwasababu alikuwa mchezaji wetu, hivyo baada ya kikao hicho tutatoa
ufafanuzi ingawa mwanzo tulizungumza naye na anafahamu kila kitu.”
CHANZO:MWANASPOTI.
0 comments:
Post a Comment